Blog

heka heka za lala salama kuelekea kilele cha tamasha la serengeti fiesta 2012 mwembe yanga leo


Mmoja wa watangazaji wa Clouds pichani kati,Antu Mandoza akiwa na baadhi ya washabiki wakubwa wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,ndani ya viwanja vya Mwenge Yanga,Temeke jijini Dar mapema leo wakati heka heka za lala salama kuelekea kwenye kilele cha tamasha hilo litakalofanyika katika viwanja vya Lidaz club,Kinondoni jijini Dar,ambapo Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani,Rick Ross atatumbuiza.
Antu Mandoza,akimhoji Mwanadada Diana mara baada ya kujishindia kiasi cha shilingi 25,000/= pamoja na fulana ya fiesta mapema leo kwenye viwanja vya Mwembeyanga, wakati heka heka za lala salama kuelekea kwenye kilele cha tamasha hilo litakalofanyika katika viwanja vya Lidaz club,Kinondoni jijini Dar,ambapo Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani,Rick Ross atatumbuiza.
 Burudani ikiendelea kutolewa kwenye viwanja vya Mwembeyanga
 Mmmoja washabiki wa tamasha la fiesta akizungumza kwa ufupi kuhusiana na tamasha hilo litakalorindima siku ya jumamosi kwenye viwanja vya Lidaz club,Kinondoni jijini Dar.
Mtangazaji wa Clouds TV,kupitia kipindi cha Mwanadaisalama,Mussa Husein pichani kulia akiwauliza maswali baadhi ya watu kwa ajili ya kujishindia zawadi mbalimbali zinazotolewa  wakati heka heka za lala salama kuelekea kwenye kilele cha tamasha hilo litakalofanyika katika viwanja vya Lidaz club,Kinondoni jijini Dar,ambapo Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani,Rick Ross atatumbuiza.
 Babu nae alikuwepo. 
Kama ujuavyo panaposhughuli ya Fiesta kila mmoja hujipatia faida kwa namna moja ama nyingine


 
 Mratibu wa kuelekea kilele cha tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Mully B pichani kushoto akibadilishana mawazo na Mussa Husein,pichani kati ni dada Diana mkazi wa Temeke aliyejishindia fulana na sh 25,000/=
 Bhaassss.
Panaposhughuli za Serengeti Fiesta  huduma kama hizi hazikosekani,kuwajali wapenzi na washabiki wake kwa namna moja ama nyingine.

Read More

TAKWIMU ZA LIGI KUU BONGO, KLABU NA WACHEZAJI WANAOONGOZA KWA MAGOLI, PAMOJA NA WA MWISHO.


.
Mwandishi Shaffih Dauda ameripoti kwamba licha ya kushika nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi mbili tu baada ya kufungwa mechi mbili na kutoka sare mechi mbili, Timu ya Polisi Moro ni moja ya timu zenye ukuta mgumu zaidi VPL ikiungana na JKT Oljoro, Simba na Azam FC ambazo kwa pamoja zimeruhusu magoli mawili tuu kutinga kwenye nyavu zao.
Azam FC ndiyo timu pekee ambayo imeruhusu magoli kuingia kwenye mechi moja tuu baada ya kukubali kutoka sare 2-2 na Toto Afrika jijini Mwanza huku ikiwa imeondoka bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa kwenye mechi tatu za ligi kuu.
Hadi kufikia raundi ya nne, Simba SC ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza pointi hata moja baada ya kucheza michezo minne na kushinda yote ambapo polisi Moro imejiwekea rekodi nyingine kwenye VPL raundi ya nne baada ya kuwa timu pekee iliyocheza mechi nne bila kufunga goli hata moja.
.
Hadi kufikia raundi ya nne ya ligi kuu ya Vodacom, kuna vilabu vinne tu ambavyo havijaruhusu kupoteza mchezo hata mmoja hadi sasa, vilabu hivyo ni Toto Africa, JKT Oljoro, Coastal Union, Simba SC na Azam FC.
JKT Ruvu Stars ndiyo iliyoruhusu magoli mengi zaidi ya kufungwa ikiwa imefungwa magoli 10 hadi sasa ikifuatiwa na ndugu zao wa Ruvu Shooting Stars walioruhusu magoli nane kama ilivyo kwa wapiganaji wa African Lyon.
Kwa upande wa magoli klabu ya Simba ndio inayoongoza ikiwa na magoli tisa na kufuatiwa na Azam FC na Yanga pia yenye magoli saba huku vilabu vya Ruvu Shooting Stars na Mtibwa Sugar vikiwa vimetikisa nyavu mara sita kila kimoja.
Wachezaji Kipre Tchetche wa Azam FC na Husein Javu wa Mtibwa na Nizar Khalfan ndiyo wanaoongoza kufunga magoli kwenye ligi kuu wakiwa na magoli matatu kila mmoja hadi hivi sasa.

Read More

TAKWIMU ZA LIGI KUU BONGO, KLABU NA WACHEZAJI WANAOONGOZA KWA MAGOLI, PAMOJA NA WA MWISHO.


.
Mwandishi Shaffih Dauda ameripoti kwamba licha ya kushika nafasi ya pili kutoka mkiani ikiwa na pointi mbili tu baada ya kufungwa mechi mbili na kutoka sare mechi mbili, Timu ya Polisi Moro ni moja ya timu zenye ukuta mgumu zaidi VPL ikiungana na JKT Oljoro, Simba na Azam FC ambazo kwa pamoja zimeruhusu magoli mawili tuu kutinga kwenye nyavu zao.
Azam FC ndiyo timu pekee ambayo imeruhusu magoli kuingia kwenye mechi moja tuu baada ya kukubali kutoka sare 2-2 na Toto Afrika jijini Mwanza huku ikiwa imeondoka bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa kwenye mechi tatu za ligi kuu.
Hadi kufikia raundi ya nne, Simba SC ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza pointi hata moja baada ya kucheza michezo minne na kushinda yote ambapo polisi Moro imejiwekea rekodi nyingine kwenye VPL raundi ya nne baada ya kuwa timu pekee iliyocheza mechi nne bila kufunga goli hata moja.
.
Hadi kufikia raundi ya nne ya ligi kuu ya Vodacom, kuna vilabu vinne tu ambavyo havijaruhusu kupoteza mchezo hata mmoja hadi sasa, vilabu hivyo ni Toto Africa, JKT Oljoro, Coastal Union, Simba SC na Azam FC.
JKT Ruvu Stars ndiyo iliyoruhusu magoli mengi zaidi ya kufungwa ikiwa imefungwa magoli 10 hadi sasa ikifuatiwa na ndugu zao wa Ruvu Shooting Stars walioruhusu magoli nane kama ilivyo kwa wapiganaji wa African Lyon.
Kwa upande wa magoli klabu ya Simba ndio inayoongoza ikiwa na magoli tisa na kufuatiwa na Azam FC na Yanga pia yenye magoli saba huku vilabu vya Ruvu Shooting Stars na Mtibwa Sugar vikiwa vimetikisa nyavu mara sita kila kimoja.
Wachezaji Kipre Tchetche wa Azam FC na Husein Javu wa Mtibwa na Nizar Khalfan ndiyo wanaoongoza kufunga magoli kwenye ligi kuu wakiwa na magoli matatu kila mmoja hadi hivi sasa.

Read More

Lowassa Awatimulia Vumbi Sitta, Membe

APANGA MAJESHI YA URAIS 2015, ASEMA MONDULI NDIYO MSULI WAKE WA KISIASA 

KAMBI zinazosigana ndani ya CCM zinaonekana kuchuana vikali katika uchaguzi wa ngazi ya wilaya ya chama hicho tawala, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, huku Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akionekana kupata mafanikio, ikilinganishwa na mahasimu wake, Benard Membe na Samuel Sitta.

 Kama ilivyo kwa Lowassa, Sitta ambaye ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Membe ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wamekuwa wakitajwa kuwa kwenye harakati za kuusaka urais, hivyo uchaguzi wa ndani wa CCM ni fursa ya kupanga safu za kufanikisha mikakati hiyo. Lowassa binafsi tayari amepita katika kinyang’anyiro hicho kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM kupitia Wilaya ya Monduli. 

Jana mbunge huyo wa Monduli alitoa kauli kali akisema kuwa wapo watu wanaovuruga CCM katika Wilaya ya Monduli na kwamba tayari amewabaini, hivyo kuahidi kwamba watashughulikiwa kisiasa. ''Yako maneno ya ovyoovyo yamekuwa yakipikwa ya kuwaandama viongozi wa CCM Monduli, yanasemwa na wakubwa fulani, yanapikwa na watu fulani wa Monduli, tunawajua. Nataka kuwaambia tumewajua na nawaambia hawatuwezi,'' alitamba Lowassa. Lowassa alisema ushindi alioupata umedhihirisha kuwa ana misuli ya kisiasa na kwamba wakazi wa Monduli ndiyo msuli huo.

 ''Kuna mzee rafiki yangu aliniambia kuwa katika kazi za siasa angalia ‘grassroots’. Watu wanakuwa ndiyo msuli wako kisiasa na mimi watu wa Monduli ndiyo msuli wangu,'' alisema. Aliendelea ''Wananchi wa Monduli mmenithibitishia hilo na nawashukuru sana kutoka kwenye ‘sakafu’ ya moyo wangu, jibu la thibitisho hilo kwangu ni utumishi uliotukuka.'' Kwa upande wake, Membe anasubiri kuparurana na vigogo wenzake katika kundi la kifo la ujumbe huo katika uchaguzi wa ngazi ya Taifa, wakati Sitta tayari ni mjumbe wa NEC akiwakilisha wabunge wa CCM katika chombo hicho kikubwa cha uamuzi ndani ya chama hicho. Matokeo katika maeneo kulikomalizika uchaguzi wa ngazi ya wilaya yanaonyesha kuwa Lowassa amefanikiwa kupanga safu yake vizuri zaidi, ikilinganishwa na wenzake hao. 

Membe anaonekana kufuata kwa karibu na Sitta ni kama anashika mkia kwa kuwa na wafuasi wachache waliofanikiwa kuchaguliwa. Hata hivyo, chaguzi katika baadhi ya mikoa bado zinaendelea, huku uchaguzi wa ngazi za mikoa na taifa ukisubiriwa kwa hamu. Manyara na Arusha Kundi la Lowassa lilizidi kupata nguvu baada ya mfuasi wake mpya ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji na Uwekezaji), Dk Mary Nagu kumbwaga Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye. Sumaye naye anatajwa kuwa miongoni mwa ‘wanaoutaka’ urais na kuanguka kwake katika uchaguzi wa Hanang, kunatia doa kubwa harakati zake hizo. 

Katika uchaguzi uliofanyika jana kwenye Wilaya ya Arusha Mjini, Lowassa ameibuka kidedea kwa wapambe wake kadhaa kuchaguliwa, huku mwenyekiti wa zamani wa CCM wa Wilaya hiyo, Jubilate Kileo akiangushwa na Dk Wilfred Ole Soilel. Katika kinyang’anyiro cha mjumbe wa Nec, Godrey Mwalusamba alishinda na kuwaangusha vibaya wapinzani wake ambao ni Loota Laiser na Dk Harold Adamson.Kuchaguliwa kwa Dk Ole Soilel anayehusishwa na kambi la Lowassa kuliibua simanzi kwa kambi nyingine ambapo katika hali isiyo ya kawaida, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo na Katibu wa CCM Arusha, Mary Chatanda walionekana kuwa wanyonge muda wote. 

Mwanza na Dodoma Mkoani Mwanza, kambi za Lowassa na Membe zinatajwa kuchuana vikali huku kukiwa na sintofahamu kwamba mgombea wa nafasi ya mweyekiti wa mkoa huo, Anthony Diallo yuko upande upi. Diallo ambaye alianguka katika uchaguzi wa ubunge Oktoba 2010, anaonekana kurejea kwa nguvu mpya, kwani tayari baadhi ya wale wanaotajwa kuwa wafuasi wake wametwaa nafasi muhimu katika uchaguzi wa wilaya. 

Hata hivyo, kada huyo wa siku nyingi wa CCM ambaye anamaliza muda wake wa ujumbe wa NEC akiuwakilisha Mkoa wa Mwanza, anakabiliwa na kibarua kigumu Oktoba 13, mwaka huu, atakapopambana na mweyekiti anayetetea nafasi yake Clement Mabina, Zebedayo Athumani na Joseph Langula Yared. Kwa sasa kuna taarifa kwamba Diallo anamuunga mkono Membe hivyo ushindi wa wafuasi wake katika Wilaya za Nyamagana, Ukerewe, Misungwi na Sengerema unaweza kuinufaisha kambi hiyo. 

 Mabina ambaye anatajwa kuwa mshirika wa Lowassa, katika matokeo ya awali, kambi yake inaonekana kutokufanya vizuri. Ushindi muhimu katika Wilaya ya Nyamagana ulikuwa ni wa nafasi ya Mwenyekiti iliyonyakuliwa na msadizi wa siku nyingi wa Diallo, Raphael Shilatu, ambaye aliwabwaga Mashaka Kaguna aliyetajwa kuwa mfuasi wa Lowassa na Yahya Nyaonge anayetajwa kuwa mfuasi wa Sitta. Hata hivyo, ushindi huo unatajwa kutiwa doa na mmoja wa wafuasi wa Lowassa ambaye ni mbunge wa zamani wa Nyamagana, Lawrence Masha ambaye alikuwa mjumbe wa NEC. 

Wilayani Ukerewe kambi ya Membe inatajwa kushinda kiti cha Uenyekiti kupitia Ally Mabile na katika Wilaya ya Busega kambi ya Sitta inatajwa kutwaa ujumbe wa NEC kupitia kwa mbunge wa zamani wa Busega, Dk Raphael Chegeni. Mkoani Dodoma matokeo ya uchaguzi wa nafasi mbalimbali yanaonyesha kwamba kambi ya Lowassa imefanya vizuri hasa katika Wilaya za Dodoma Mjini, Bahi, Kondoa, Chemba na Kongwa. 

Hata hivyo, ngome ya Waziri Mkuu huyo wa zamani imeangukia pua katika Wilaya ya Chamwino, baada ya wapambe wake kubwagwa na wale wanaotajwa kumuunga mkono Sitta. 

Katika Wilaya ya Mpwapwa viongozi waliochaguliwa ni wapya na hadi sasa haifahamiki wanaunga mkono kambi gani. Dar, Zanzibar na Moro Visiwani Zanzibar, Lowassa aliendelea kupeta kutokana na ushindi wa aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM), Hamad Yussuf Masauni, ambaye alishinda nafasi ya ujumbe wa NEC na kumbwaga aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo, Mahamoud Thabiti Kombo. 

 Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Katibu wa Wilaya ya Mjini, Fatma Juma Shomari alisema kwamba kati ya wagombea 19 waliokuwa wakiwania nafasi sita za NEC, Masauni aliibuka mshindi wa pili akitanguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai. Aliyeshinda nafasi ya uenyekiti ni Juma Faki Chumu na wajumbe wengine wa NEC ni Buruhani Saadati Haji, Asha Abdalla Juma, Talib Ali Tali Sufiani Khamis Ramadhani na Omar Jastus Morris. 

 Hata hivyo, katika Mkoa wa Dar es Salaam, kambi ya Lowassa ilipata pigo kutokaana na kubwagwa kwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga aliyekuwa akiwania nafasi ya ujumbe wa NEC kupitia Wilaya ya Ilala. Kadhalika mkoani Morogoro, kambi hiyo pia ilipata pigo kutokana na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makala kubwagwa na Suleiman Ahmed Sadiq katika uwakilishi wa NEC Wilaya ya Mvomero.

 Taarifa kutoka mkoani Tabora zinasema katika wilya zote za mkoa huo, kambi ya Lowassa imeshinda kwa kishindo isipokuwa Wilaya ya Urambo ambayo kambi ya Sitta inadaiwa kuibuka kidedea. Wasomi wanena Baadhi ya wasomi nchini, wametofautiana kimtazamo kuhusu chaguzi ndani ya CCM huku wengine wakisema chama hicho kimeshindwa kuwadhibiti vigogo wanaotajwa kuwania nafasi ya urais ambao wamefanikiwa kuwaingiza wafuasi wao kwenye nafasi mbalimbali za uongozi. 

Mhadhiri wa Chuo cha Kumbukumbu cha Mwalimu Nyerere, Sabun Parit alisema hatma ya chama hicho kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao ni nzuri kutokana na kufanikiwa kuendesha uchaguzi wake kwa utulivu. “Mara nyingi tumezoea kuona makundi yakiibuka wakati wa uchaguzi, lakini safari hii hali ni shwari, hatujasikia makundi wala malalamiko na hii ni ishara kwamba hiki chama kimekomaa na hakiwezi kutetereka,” alisema mhadhiri huyo. 

 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Kitilya Mkumbo ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alisema jana kuwa CCM imeshindwa kuwadhibiti vigogo hao ndani ya chama hicho na hivyo wameanza vizuri katika maandalizi ili kupitishwa na chama hicho kugombea kiti ya urais. “Kwa kweli CCM wamejimaliza na wameonekana kuwa hawana jipya, wale waliotaka kuwavua magamba ndiyo haohao wamepitishwa kwenye uchaguzi pamoja na wafuasi wao kuwasaidia katika Uchaguzi Mkuu,” alisema Dk Mkumbo. 

Naye Mhadhiri wa UDSM, Dk Benson Bana alisema CCM imeonyesha kwamba hakuna kiongozi yeyote mwenye hatimiliki ya chama hicho. “Kwa namna mambo yalivyoonyeshwa kwenye uchaguzi huo, mtu yeyote anaweza kuingia na kuondoka kwenye chama hicho,” alisema. 

Naye Kisena Mabuba ambaye pia ni Mhadhiri katika Chuo cha Mwalimu Nyerere alisema uchaguzi huo umefuta makundi ndani ya CCM. “Tofauti na matarajio ya wengi kuwa CCM ingemeguka, mimi ninachokiona hapa kundi lililobaki na nguvu ni lile la mwenyekiti mwenyewe. Kundi moja limefutwa kabisa na mengine yameshindwa kupata nguvu za kutosha,” alisema Mabuba.

 Alitaja mbinu zilizotumika kufuta makundi hayo kuwa ni hatua ya kubadili katiba na kuwaweka pembeni marais wastaafu pamoja na uteuzi wa makatibu wa chama ngazi ya mikoa na wilaya ambao walifanya makundi kupoteza nguvu. 

 Habari hii imeandikwa na Moses Mashalla (Arusha), Habel Chidawali (Dodoma), Frederick Katulanda (Mwanza) na Joseph Zablon, Raymond Kaminyoge na George Njogopa.MWANANCHI

Read More

Lowassa: Tuko tayari kuingia vitani na Malawi....!





Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama,Edward Lowassa
Reginald Simon na Daniel Mjema, Dodoma
KAMATI ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imesema Tanzania imejiandaa kiakili na kivifaa kuingia vitani na Malawi kama italazimika kufanya hivyo.Akizungumza mjini Dodoma jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Edward Lowassa alisema kamati yake imeridhishwa na maandalizi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

“Tumepewa maelezo na jeshi letu na tumeridhika kuwa ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na limejipanga vizuri sana kwa uhakika, kiakili na kivifaa,” alisema Lowassa.

Kabla ya Lowassa kuzungumza na waandishi wa habari, alifanya kikao cha faragha kilichohusisha pia wajumbe wa kamati hiyo na makamanda wa JWTZ walipofika bungeni kutoa taarifa kwa kamati hiyo.
Hata hivyo, katika tamko hilo Lowassa alisema Tanzania inatarajia mgogoro huo utamalizika kwa njia za kidiplomasia kwa sababu Watanzania na Wamalawi ni ndugu wa muda mrefu.
“Ikibidi kuingia vitani jeshi letu liko vizuri sana na kama ilivyo ahadi yao (JWTZ), wako tayari kulinda mipaka ya nchi yetu hadi tone la mwisho. Tunasali sana tusifike hapo,” alisema Lowassa na kuongeza: “Tunategemea hatutafika huko, lakini kwa heshima ya nchi yetu kama ikibidi kufika huko (vitani) tutafika kulinda mipaka yetu”.
Mwenyekiti huyo ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu, alisema kama Tanzania itafikishwa mahali itabidi damu ya Watanzania imwagike, nchi iko tayari kulinda mipaka yake kwa nguvu.Alisema kama itabidi kuingia vitani, itatumia umoja na mshikamano wa Watanzania wa mwaka 1978 wakati wa Vita na Uganda kulinda mipaka ili kulinda heshima ya nchi.
Alisema mwaka 1978 wakati Rais wa Uganda, Idd Amin na majeshi yake walipochukua sehemu ya Tanzania na kujitangazia ni mali yake, ilichukua hatua kumfukuza Amin.
“Alijitangazia sehemu ile ni mali ya Uganda hutegemei nchi ikae kimya, hutegemei Watanzania wanyamaze wakati nchi yao imetekwa, tulichukua hatua tukamfukuza hadi nchini kwake.”
Lowassa alisema Kamati ya Bunge inajua madhara ya kiuchumi yaliyotokana na Vita ya Idd Amin na kwamba vita yoyote ikipiganwa lazima kunakuwa na madhara ya kiuchumi.
Hata hivyo, alisema anaamini mgogoro huo hautafika huko na kusisitiza kuwa, lakini ikibidi JWTZ ni moja kati ya majeshi bora duniani na ni jeshi lililojiandaa vizuri kwa lolote.
“Wako tayari sisi ni moja kati ya jeshi lililojiandaa vizuri na jeshi bora duniani na la kujivunia. Tuko imara kiakili na kivifaa tena vya kisasa,” alisema Lowassa.
Alisema kamati yake inaunga mkono msimamo ulitolewa bungeni juzi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe kuhusu mgogoro huo na kwamba ndiyo kauli rasmi ya Serikali.
Juzi, Waziri Membe alizionya kampuni za kigeni za Malawi zilizoingia katika ardhi ya Tanzania eneo la Ziwa Nyasa kutafiti mafuta na gesi kusitisha mara moja.
Akiwasilisha makadirio ya wizara yake, Membe alisema upo ushahidi kuwa ndege tano za utafiti za Malawi ziliruka anga la Tanzania na kutua katika Ziwa Nyasa upande wa Tanzania.Membe alisema pamoja JWTZ kutoruhusu ndege hizo za Malawi kuingia na kutua eneo hilo la Ziwa Nyasa, bado ziliingia na kutua kinyume kabisa cha sheria za kimataifa.
“Wenzetu wa Malawi wanadai Ziwa Nyasa lote lipo Malawi na msingi wa madai yao ni mkataba wa Heligoland wa mwaka 1890 na sisi tunasema mpaka uko katikati ya Ziwa.”
Membe alisema hata mgogoro wa mpaka kati ya Cameroon na Nigeria ulitatuliwa na Mahakama Kuu ya Dunia kuwa mpaka baina ya nchi hizo mbili upite katikati ya Ziwa Chad.
Juzi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Patrick Kabambe alikaririwa na Redio Sauti ya Ujerumani akisema wataendelea na utafutaji mafuta licha ya onyo hilo la Tanzania.
Waziri huyo alisema ziwa hilo linaitwa Malawi na siyo Ziwa Nyasa na kwamba utafutaji wa mafuta na gesi utaendelea na hakuna wa kuwasimamisha. Alihoji, iweje Tanzania ishtuke sasa?

Read More

TANZANIA YAKOPESHWA SH.BILIONI 280


Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa

Serikali kupitia Wizara ya Fedha imepewa mkopo wa Sh. bilioni 280, ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji katika jiji la Dar es Salaam na maeneo ya Chalinze, mkoani Pwani.

Akisaini mkopo huo jana jijini Dar es Salaam na Meneja Mkuu wa Benki ya Exim ya India, Geeta Poojary, Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa, alisema mkopo huo umekuja kwa wakati ili kusaidia Tanzania kukabiliana na tatizo hilo kwa kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi kwa wakazi wa maeneo husika.

“Badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji, ni vyema wakazi wa maeneo hayo kupitia mkopo huu kujiongezea kipato na kukabiliana na umaskini,” alisema.

Aidha, Dk. Mgimwa alisema mradi huo utasaidia kuongeza uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo milioni 82 hadi milioni 196 kwa siku.

“Mradi huu utahusisha ujenzi wa njia ya usafirishaji wa maji na kuongeza mtandao wa usambazaji kwa mteja,” alisema Waziri huyo na kuongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo itakuwa ni sehemu ya kutekeleza mkakati wa kukuza Uchumi na Kupunguza Umasilini (Mkukuta) na kupunguza magomjwa yanayotokana na maji yasiyokuwa salama.

Alisema mkopo huo ni moja ya mikopo nafuu sana kwani Tanzania itatakiwa kulipa riba ya asilimia 1.7.

Read More

KESI YA LEMA MAWAKILI WALUMBANA

Aliyekuwa  mbunge wajimbo la Arusha Mjini Godbless Lema akiwasalimu wanachama mara baada ya kutoka mahakamani
Malumbano ya mawakili jana yalitawala kesi ya rufani iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Godbless Lema.

Wakili wa Lema, Method Kimomogoro aliiambia mahakama kuwa iwapo madai ya wakili ya wajibu rufani, Alute Mughwai kwamba hati ya kukazia hukumu iliyomvua ubunge Lema, ni batili, basi mteja wake ni mbunge halali.

Kimomogoro alitoa madai hayo jana wakati akijibu pingamizi la awali lililotolewa na wakili Mughwai, aliyedai kwamba hati hiyo ina kasoro kubwa za kisheria ambazo inafanya rufani hiyo kuwa batili tangu mwanzo hadi mwisho wake.

Kutokana na hoja hiyo, Kimomogoro aliiomba Mahakama ya Rufani ifute mapingamizi yaliyotolewa na Mughwai.

Wakili Kimomogoro alitoa ombi hilo mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani wakiongozwa na Jaji Mkuu, Mohammed Othman Chande, ambaye anasaidiana na majaji Natalia Kimaro na Salum Massati.

Pia, aliomba wajibu rufani walipe gharama za kuendesha kesi. “Tunaomba mapingamizi hayo yatupiliwe mbali na walioleta wawajibike kulipa gharama na kama mtaona inafaa basi kila upande ubebe mzigo wake iwapo hoja yao itazingatiwa,” alidai Kimomogoro.

Rufani ya kesi hiyo iliyosikilizwa jana katika Mahakama Kuu Arusha,  ilikuwa ikisikilizwa pingamizi la awali, lililowasilishwa na wakili wa wajibu rufani, kwa niaba ya wateja wake, Musa Mkanga, Agnes Mollel na Hapines Kivuyo, ilivuta umati mkubwa wa watu kutoka karibu kila kona za jiji la Arusha.

Mapema wakili Mughwai alitaka rufani hiyo ifutwe kwa kuwa hati ya kukazia hukumu ilikuwa ina kasoro mbalimbali. Pia alitaka waomba rufani walipe gharama ya kesi hiyo pamoja na gharama za mawakili kwani wameihangaikia sana kesi hiyo.

“Rufaa ambayo ipo mbele yenu ni batili kwa sababu imesimikwa kwa hati ya amri ya Mahakama Kuu ambayo ni batili, hiyo hati ni batili toka mwanzo hadi mwisho wake,” alidai.

Aliendelea kuiambia mahakama kuwa kukosekana kwa muhuri wa mahakama katika hati hiyo ni hitilafu kubwa hata kama hati yenyewe ina saini ya jaji aliyeiandika.

Alidai kuwa uwepo wa muhuri wa mahakama unaonyesha mamlaka na uhalali na nyaraka yenyewe na kwamba bila muhuri nyaraka hiyo ni karatasi ya bure.

Mughwai hakukubaliana na hoja ya waleta rufaa kwamba hawahusiki na kasoro hizo isipokuwa  wanaohusika ni mahakama kwani wao walitakiwa kujiridhisha kwamba hati hiyo imekamilika.

Katika hoja nyingine ya pingamizi, Mughwai alidai kuwa hati hiyo haionyeshi tarehe iliyotolewa ingawa ipo tarehe iliyoandikwa.

Aliieleza kuwa utaratibu huo unakwenda kinyume cha Kanuni ya 9 ya Masjala ya Mahakama Kuu na kuongeza kuwa hati hiyo haikuandikwa kwa muundo unaotakiwa kwa mujibu wa kanuni na sheria.

Akijibu mapingamizi hayo, Kimomogoro alidai kuwa mazingira ya shauri hilo yalikuwa ya kipekee baada ya kutolewa hukumu Mahakama Kuu na kwamba jalada la kesi lilipelekwa Dar es Salaam, kwa hiyo hawakuwa na nafasi ya kuangalia hati hiyo.

Aliongeza kuwa wakili Mughwai katika pingamizi amekwepa au kuchenga kwa makusudi kuelezea kanuni mpya na uamuzi wa kesi zilizotolewa siku za hivi karibuni kwa kuzingatia kanuni hizo kuelezea haki za msingi.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Timon Vitalis, ambaye katika kesi hiyo anamwakilisha Mwanasheria Mkuu, lakini kama sehemu muhimu (necessary party) alimuunga mkono wakili Kimomogoro, kwa hoja kwamba hati ya kukazia hukumu inatolewa chini ya Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai (CPC) na  siyo chini ya Kanuni ya Masjala ya Mahakama Kuu, hivyo alitaka kama kuna mgongano basi CPC ndiyo itumike.

“Hata ukisema hati ya kukazia hukumu ina kasoro, basi anayepaswa kulaumiwa ni mamlaka iliyotoa hati hiyo na siyo wakili wa waomba rufani, hivyo mahakama ina jukumu la kutoa hati iliyo sahihi,” alidai.

Baada ya kusikiliza pande zote mbili, Jaji Mkuu Chande, aliahirisha kesi hiyo hadi tarehe nyingine ambayo watapanga.

“Uamuzi utatolewa kwa tarehe ambayo mtaarifiwa,”  alisema Jaji Chande.

Aprili 5, mwaka huu, Mahakama Kuu Tanzania Kanda Arusha,  ilitengua matokeo ya ubunge yaliyompa ushindi Lema baada ya kuridhika kuwa alitumia lugha ya kashfa na udhalilishaji dhidi ya aliyekuwa mpinzani wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Dk. Batilda Burian.

Hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Gabriel Rwakibarila, baada ya kumtia hatiani Lema kwa makosa mawili kati ya manne aliyokuwa akikabiliwa nayo, huku akitupa mawili kwa kukosa ushahidi.

Jaji Rwakibarila alimvua ubunge Lema baada ya kuridhika na ushahidi kuwa alitumia maneno ya kashfa na ubaguzi wa jinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Burian.

Pia Jaji Rwakibarila katika hukumu yake hiyo, alimwamuru Lema kulipa gharama za kesi hiyo.

Hata hivyo, alimweleza kuwa ana haki ya kukata rufaa ikiwa ataona hakuridhika na hukumu hiyo.



Read More

Recent Posts

Latest Tweets

Flickr Photostream